Exodus 6:18-22

18 aWana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133.

19 bWana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao.
20 cAmramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Haruni na Musa. Amramu aliishi miaka 137.
21 dWana wa Ishari walikuwa Kora, Nefegi na Zikri.
22 eWana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elisafani na Sithri.
Copyright information for SwhKC